Baada ya kukamilisha mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar hapo jana, kikosi cha Yanga kinaelekea mkoani Iringa kwa ajili ya mchezo wa kukamilisha msimu dhidi ya Lipuli Fc
Mchezo huo utapigwa Jumapili, Julai 26 kwenye uwanja wa CCM Samora
Mchezo huo ndio utakaotoa hatma ya nafasi ya pili inayowaniwa na vilabu vya Yanga na Azam Fc
Leo Azam Fc itacheza na Mbeya City, ikipata ushindi itaiondoa Yanga katika nafasi ya pili kutokana na wingi wa mabao
Wakati Yanga itakamilisha msimu dhidi ya Lipuli, Azam watakamilisha msimu dhidi ya Tanzania Prisons
ADVERTISE HERE