Mlind alango kinda Ramadhani Kabwili jana alicheza mchezo wake wa kwanza msimu huu kwenye ligi akianza dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Kabwili amedhihirisha, hajachuja na pengine anastahili kupewa nafasi ya kucheza mechi zaidi
Ulikuwa ni mchezo wenye presha kubwa lakini Kabwili alionyesha utulivu wa hali ya juu na akatimiza majukumu yake vile alivyopaswa
Katika mchezo huo Faroukh Shikhalo ndiye aliyekuwa kocha wake kutokana na kukosekana kwa Peter Manyika ambaye ilielezwa kuwa alipata msiba
Shikhalo aliumia siku chache kabla ya mchezo dhidi ya Mwadui Fc, alianza mazoezi mepesi siku moja kabla ya safari ya Morogoro wakati Metacha Mnata nae ni Mgonjwa
Hakuna shaka, Kabwili ni hazina kubwa kwa Yanga!
ADVERTISE HERE