Kitu pekee ambacho kinaweza kumbeba kocha Luc Eymael kuendelea kuinoa Yanga ni mapungufu ya kikosi na sio matokeo
Tangu atue Yanga mwezi Januarry, Eymael amewaongoza mabingwa hao wa kihistoria katika michezo 26
Amefanikiwa kushinda michezo 11, sare michezo 12 na vipigo mara 3, amepata wastani wa matokeo ya sare zaidi katika michezo aliyoongoza
Msimu ndio unamalizika, tusubiri kuona nini atafanya wakati wa maandalizi ya msimu ujao, wengi watahitaji kuona anapindua matokeo haya kwa kupata ushindi zaidi
Hatakuwa na utetezi kama mambo hayatamnyookea kwani atakuwa na kikosi ambacho amekipendekeza mwenyewe
ADVERTISE HERE