Klabu ya Mbao FC inasaka saini za chipukizi wa Yanga, Edward Maka na Yusufu Mhilu kujiunga na timu hiyo kwa mkopo.
Taarifa zinasema kuwa Mbao iliomba Yanga kuwapa wachezaji hao kwa mkopo, maombi ambayo bado hayajajibiwa na uongozi wa Yanga.
Katibu Mkuu wa Mbao, Daniel Naila licha ya kutokubali moja kwa moja kama waliomba wachezaji hao, amesema kwa sasa wanaangalia mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Majimaji utakaopigwa kesho Jumamosi mjini Songea.
Ameongeza kuwa kama Kocha atakuwa amewaona na kuvutiwa nao, ataongea naye kama anawahitaji kisha baada ya mchezo atatoa taarifa rasmi.
"Huenda alishawaona na kuvutiwa nao, ila kwa sasa tunapambana na mchezo wa Jumamosi na Majimaji, kwahiyo tukimaliza nitaongea naye kocha na sisi kama uongozi tupo tayari kutekeleza" alisema Naila.
Kwa hisani ya Mwanaspoti

ADVERTISE HERE