Inaelezwa tayari uongozi wa Yanga unayo orodha ya wachezaji ambao wataachwa na timu hiyo pale ligi itakapofika tamati siku ya Jumapili
Pamoja na hitaji ya maboresho, Yanga haitafanyau usajili wa timu nzima, kama wengi wanavyofikiria, sio zaidi ya wachezaji saba ambao wataachwa
Aidha, kulingana na taarifa kutoka ndani ya uongozi, wachezaji wapya nao hawatazidi saba, wanne wakiwa tayari mchakato wao wa usajili umekamilika
Yanga imepania kukamilisha usajili mapema ili wachezaji wapate muda wa kutosha kuwa kambini pamoja kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao
Kocha Luc Eymael ametaka aletewe 'majembe saba' ambayo yataingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza
Kwa maana wachezaji wote wapya watakaosajiliwa, hakuna hata mmoja wa kukaa benchi, uwezo wao uko juu kulinganisha na wachezaji waliopo