Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Simon Patrick ametoa maoni yake juu ya umuhimu wa kuundwa kwa Mahakama ya Ndani Maalumkwa ajili ya kusuluhisha masuala ya michezo kama ilivyo Mahakama ya Kimataifa ya Michezo (CAS)
Alichoandika Simon;
"CAS - Court of Arbitration for Sports, ni mahakama ya kimichezo yenye makao makuu yake kwenye mji wa Lausanne, Switzerland.
"Kazi kubwa ya mahakama hii ni kusikiliza mashairi dhidi ya Vilabu, shirikisho la mpira, vilabu, wachezaji, mawakala na wadau mbali mbali wa mpira wa miguu duniani.
"Mahakama hii pia hutumika kama mahakama ya rufaa dhidi ya maamuzi yote yaliyofanywa na shirikisho la mpira la nchi yoyote mwanachama wa FIFA pamoja na maamuzi ya FIFA Dispute Resolution Chamber.
"Waamuzi wa CAS huchaguliwa na walalamikaji wa kesi husika, wakishindwa kufanya hivo, Rais wa CAS huchagua waamuzi ambao hawana maslahi yoyote dhidi ya kesi husika na waamuzi hao weredi wa hali ya juu katika maswala ya kisheria, hii husababisha mahakama hii kua kimbilio la wanyonge duniani.
"Nchi mbali mbali duniani zimechukua muundo huu wa CAS na wa FIFA Dispute Resolution Chamber kwenye vyombo kuanzisha vyombo vyao vya haki katika nchi zao, naiombea nchi yangu iwe moja ya nchi ambazo inaiga muundo huu wa haki katika michezo, hii itasaidia sana kuinua haki kwenye michezo Tanzania, hili halimuhitaji JPM, sisi wenyewe tunaweza kulifanya"