Mapema leo, Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael aliongoza msafara wa Yanga mkoani Morogoro benchi lake la ufundi likiwajumuisha Cassim Fareed, Redoh Burden, Abeid Mziba, Said Maulid, Fred Mbuna na Dr. Shecky Mngazija
Kwa mara ya kwanza kocha Msaidizi Charles Mkwasa na kocha wa makipa Peter Manyika hawakujumuishwa katika msafara huo kwa kile kilichoelezwa kutokuwepo kwa maelewano kati yao na kocha mkuu
Aidha, kulingana na taarifa iliyotolewa na Yanga, Wachezaji walioondoka katika msafara ni pamoja na Farouk Shikhalo, Metacha Mnata, Ramadhan Kabwili na Geoffrey Magaigwa, Juma Abdul, Paul Godfrey, Ally Mtoni, Jafary Mohammed, Adeyum Saleh na Lamine Moro.
Wengine ni Faisal Salum, Abdullaziz Makame, Said Juma Makapu, Deus Kaseke, Mrisho Ngassa, Eric Kabamba Yikpe Gislain, David Molinga, Tariq Seif, Ditram Nchimbi na Adam Kiondo
Viongozi wengine waliojumuishwa kwenye msafara huo ni Mike Victor, Edward Martine Fungameza, Laurent Mmassy na Mkuu wa msafara Hassan Bumbuli pamoja na Dereva Sadick Bura
Yanga tayari imewasili Morogoro kuwakabili Mtibwa Sugar katika mchezo ambao utapigwa keshokutwa Jumatano