Niyonzima, Balama kukosa mechi zilizobaki kukamilisha msimu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jul 2020
Niyonzima, Balama kukosa mechi zilizobaki kukamilisha msimu

Yanga imeelekea mkoani Morogoro bila ya kiungo Haruna Niyonzima ambaye kwa mujibu wa kocha Luc Eymael atakosa michezo yote miwili iliyobaki kutokana na majeraha yanayomsumbua

Niyonzima alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Biashara United, alicheza mchezo dhidi ya Simba akiwa na majeraha

"Niyonzima hatacheza mechi zilizobaki, ameungana na Balama (Mapinduzi) ambaye yuko nje kwa wiki kadhaa. Pengine Shikhalo naye hatoweza kucheza pia kutokana na majeraha aliyopata mazoezini. Nadhani wachezaji hawa watajiunga nasi tutakapoanza maandalizi ya msimu mpya," amesema Eymael

Yanga inakabiliwa na mechi mbili ngumu za kukamilisha msimu kwani inakwenda ugenini kupambana na timu zilizo katika hatari ya kuteremka daraja

Wanaanza na Mtibwa Sugar keshokutwa Jumatano kisha kuelekea Iringa kuifuata Lipuli Fc kwa ajili ya mchezo wa kukamilisha msimu ambao utapigwa Jumapil ijayo

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’