Ukweli ni kuwa matokeo ambayo Yanga imeendelea kupata hayapaswi kuwashangaza wanayanga kwani wanafahamu sababu iliyopelekea haya kutokea
Shukrani za kipekee wanastahili GSM ambao waliingia kuokoa jahazi baada ya kuona mambo yanazidi kwenda mrama.
Kama sio wao,Β pengine Yanga ingekuwa kwenye vita ya kupigania kubaki ligi kuu
Hali ilikuwa mbaya zaidi ya ilivyo sasa. Wachezaji hawakuwa walilipwa mishahara kwa wakati na tena wengine waliamua kuvunja mikataba yao na kuondoka, wengine wakikosa morali ya kucheza
Uongozi wa Yanga chini ya Dk Mshindo Msolla tayari umefanya jambo moja kubwa kwa kushirikiana na GSM ambao wameonyesha dhamira ya dhati kuifanya Yanga ijitegemee
Ni kuanza kwa mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji. Mchakato huu ukikamilisha utawezesha timu kujitegemea na pengine kumaliza changamoto zote za kiuchumi zinazoikabili timu
Kuwa na timu imara kunahitaji fedha, hakuna Mdhamini/Mwekezaji ambaye atakuwa tayari kutoa fedha zake sehemu ambayo haina mpangilio.
GSM wameonyesha nia ya kutaka kuwekeza Yanga lakini ni muhimu timu iwe na mfumo unaoleweka ambao utawahakikishia GSM usalama wa fedha zao na hata wawekezaji wengine watakaokuja
Hawa akina Dk Msolla ndio walioanzisha mchakato huu, kwa maoni yangu tuwaache wakamilishe kisha tutawahukumu huko mbele kama mambo hayatabailika kwani sote tunafahamu sababu ya timu yetu kutokuwa bora kwa miaka ya karibuni ni ukosefu wa fedha