Mshambuliaji Mtanzania Yusuph Soka anayecheza soka la kulipwa nchini Sweden, ni miongoni mwa wachezaji wanaofanya mazoezi na katika kikosi cha Yanga
Soka anayechezea klabu ya ligi daraja la pili huko Sweden IFK Ostersund, alishiriki mazoezi ya jana chini ya kocha Luc Eymael
Bado haijafahamika kama nyota huyo anaweza kuwa miongoni mwa wachezaji wanaoweza kusajiliwa, lakini hakuna shaka Eymael ameonyesha kuvutiwa nae
Kama ilivyokuwa kwa Abdallah Shaibu 'Ninja', Soka alijumuishwa kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria ambao walikuwa wakijiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc
Soka mwenye umri wa miaka 25, aliwahi kutamba na klabu ya African Lyon miaka michache nyuma kabla kupata nafasi ya kwenda kusakata kabumbu huko Sweden
ADVERTISE HERE