Nahodha ya Yanga Papy Tshishimbi amesema kocha Luc Eymael alilazimika kumchezesha mechi dhidi ya Simba licha ya kuwa hakuwa fiti
Tshishimbi amesema anazipokea lawama za mashabiki wanaodai kuwa hakuwa katika kiwango bora lakini alilazimika kucheza baada ya kocha Luc Eymael kumtaka acheze
Mcongomani huyo amesema kipigo walichopokea kutoka kwa watani zao bado kinamuuna na inafaa iwe sababu kwa viongozi kuimarisha timu kuelekea msimu ujao
"Nafahamu wapo wanaonilaumu kuwa sikuwa katika kiwango kizuri lakini ni kocha aliyeniomba niingie uwanjani kucheza mchezo ule"
"Nilifahamu sikuwa vizuri uwanjani lakini sikuwa na namna, nililazimika kucheza kutokana na hali ya kikosi ilivyokuwa"
"Mashabiki wetu wafahamu hatuna furaha na kile kilichotokea kwenye mchezo ule, kwa niaba ya wachezaji wenzangu nitumie fursa hii kuwaomba radhi, tulifanya makosa makubwa katika mchezo ule. Soka ni mchezo wa makosa , tulikosea tukaadhibiwa. Sasa turudi kuwa wamoja ili safari iendelee," Tshishimbi alinukuliwa na Mwanaspoti
Tshishimbi aliongeza kuwa ni vyema uongozi ukafanyia kazi changamoto zilizoonekana ili kuimarisha kikosi lakini pia ni vyema wakachukua hatu thabiti kusimamia suala la nidhamu kwa wachezaji