FT : Yanga 3-1 Singida United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jul 2020
FT : Yanga 3-1 Singida United

Yanga imefanikiwa kuondoka na alama zote tatu uwanja wa Taifa leo baada ya kuichapa Singida United mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa majira ya saa moja usiku

Ulikuwa mchezo ambao Yanga ilihitaji kushinda kupunguza presha ya mashabiki kufutia kipigo cha aibu kutoka kwa watani zao mapema wiki hii

Winga Mrisho Ngasa alikuwa na mchango mkubwa kwenye ushindi wa mabingwa hao wa kihistoria akifunga bao moja na kutengeneza jingine

Beki Paulo Godfrey 'Boxer' ambaye kwa mara ya kwanza leo alijumuishwa kwenye kikosi na kocha Luc Eymael ndiye alianza kuifungia Yanga bao la kuongoza baada ya kumalizia mpira uliogonga mwamba baada ya shuti la Raphael Daudi

Ngasa aliweka kambani bao la pili wakati Yikpe Gnaniem leo alifunga bao safi akimpiga chenga mlinda lango wa Singida United Owen Chaima

Yikpe angeweza kuondoka na mpira leo kama angekuwa makini kutumia nafasi nyingi alizopata

Ushindi umeirejesha Yanga kwenye nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 67 baada ya Azam Fc kuchapwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar

Mchezo unaofuata ni dhidi ya Mwadui Fc na utapigwa Jumamosi, Julai 18

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
26m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’