Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa watani zao Simba kimewapa taswira halisi ya aina ya usajili ambao wanapaswa kufanya kuelekea msimu ujao
Mbelgiji huyo amesema matokeo hayo yamewaumiza lakini anaamini yatawasaidia kusahihisha makosa katika usajili wa kukiimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao
"Nadhani kila aliyefuatilia ule mchezo aligundua mapungufu yetu yako wapi na sasa tunapaswa kuyarekebisha ili kuhakikisha msimu ujao tunakuwa na timu yenye ushindani"
"Tunapaswa kuwa makini kwenye usajili. Tunahitaji wachezaji bora watakaoweza kushindana na timu nyingine. Nimezungumza na viongozi kuhusu mkakati wa usajili na aina ya wachezaji ambao tunapaswa kuwa nao. Tutazungumza tena baada ya ligi kumalizika. Hatupaswi kurudia makosa " alisema Eymael
cutUnaweza kusema usajili wa Yanga msimu huu unaomalizika ulikuwa wa 'kuunga-unga'. Idadi kubwa ya wachezaji waliosajiliwa na Mwinyi Zahera, kocha wa zamani wa mabingwa hao wa kihistoria waliachwa mwezi Januari, wakasajiliwa wachezaji wengine
Hata hivyo usajili huo bado umeshindwa kuifanya Yanga kuwa katika ubora na hivyo kushindwa kutimiza malengo waliyojiwekea
Eymael amesema wachezaji wote ambao watasajiliwa kuelekea msimu ujao lazima wakidhi vigezo ambavyo vitawekwa
Dirisha la usajili litafunguliwa wiki mbili zijazo, kuanzia August 01 na litafungwa August 31
Huenda kukashuhudiwa mabadiliko makubwa ya kikosi cha Yanga, wadhamini/wahisani GSM wakitenga zaidi ya Tsh Bil 1.5 kwa ajili ya zoezi la usajili