Mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga saa moja usiku wa leo watashuka kwenye uwanja wa Taifa kuumana na Singida United katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 35
Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga kuondoka na alama zote tatu kubaki katika mbio za kuwania nafasi ya pili
Watacheza na Singida United ambayo tayari imejihakikishia kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao
Kutokana na mwenendo wa Singida United, matumaini ya wengi ni kuona Yanga ikiondoka na ushindi mnono, matokeo tofauti yanaweza kumuweka matatani kocha Luc Eymael ambaye kwa hakika atakuwa kwenye presha kubwa hasa baada ya kikosi chake kubugizwa mabao 4-1 na Simba kwenye mchezo uliopita
Eymael huenda akafanya mabadiliko ya kikosi chake kilichocheza juzi, akiwapa nafasi wachezaji ambao hawakujumuishwa kwenye mchezo huo
Mabingwa hao wa kihistoria watawakosa baadhi ya wachezaji ambao kulingana na takwimu, wamefikisha idadi ya kadi tatu za njano
Wachezaji hao ni Feisal Salum, Said Juma na Juma Abdul
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo, kuiunga mkono timu yao na kusahau matokeo ya mchezo uliopita kwani maisha lazima yaendelee