Kikosi cha Yanga kitashuka kwenye dimba la Uhuru Jumapili, Novemba 19 kuivaa Mbeya City kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 10.
Baada ya sare mbili mfululizo dhidi ya Simba na Singida United, ushindi ni matokeo yanayohitajiwa zaidi na Yanga dhidi ya Mbeya City.
Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 17 wakati Mbeya City iko nafasi ya saba ikiwa na alama 11 kwenye msimamo wa ligi.
Safu ya ushambuliaji ya Yanga itaendelea kuwategemea Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa ambao kwa pamoja wameshirikiana kuifungia Yanga mabao nane kati ya 11 iliyofunga msimu huu.
Chirwa aliibuka kuwa mchezaji bora wa VPL mwezi Oktoba ambapo leo Alhamisi alikabidhiwa zawadi yake ya Tsh Mil moja na wadhamini wa ligi hiyo, Kampuni ya Vodacom.
Licha ya kuanza mazoezi mepesi, Amissi Tambwe hatarajiwi kuwa tayari kurejea dimbani kwenye mchezo huo huku Thabani Kamusoko nae akiwa ameanza mazoezi lakini hakuna uhakika juu ya utimilifu wake.
Hakuna taarifa juu ya mshambuliaji Donald Ngoma ambaye bado hajarejea kutoka kwao nchini Zimbabwe.
Papi Kabamba Tshishimbi alikumbwa na malaria, lakini Daktari wa Yanga Dk Edward bavu amesema mchezaji huyo huenda akawa tayari kuivaa Mbeya City.
Iwapo Tshishimbi na Kamusoko watashindwa kushuka dimbani kwenye mchezo huo Yanga italazimika kuwategemea Pato Ngonyani, Raphael Daudi na pengine Said Juma 'Makapu' kwenye sehemu ya kiungo.
Habari njema ni kwamba dirisha la usajili limefunguliwa jana Novemba 15 hivyo Kamati ya usajili ya Yanga inayoongozwa na Hussein Nyika itakuwa 'busy' sokoni kutafuta wachezaji wa kuongeza nguvu kwenye kikosi.

ADVERTISE HERE