Tusione aibu, kushindwa ni njia ya mafanikio - Molinga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jul 2020
Tusione aibu, kushindwa ni njia ya mafanikio - Molinga

Wakati Yanga ikijiandaa kuivaa Singida United leo katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Taifa, mshambuliaji wa timu hiyo David Molinga amewataka mashabiki wa timu hiyo kusahau matokeo ya mchezo wao dhidi ya Simba na kuendelea kuiunga mkono timu yao

Molinga amesema Wanayanga hawapaswi kuona aibu kushindwa kwani wakati mwingine hulazimika kupita hatua hiyo ili kuweza kufanikiwa

"Usione aibu unaposhindwa, kwa maana hulazimika kushindwa ili ufanikiwe. Kama unaogopa kushindwa ama kukosea basi tambua hutoweza kufanikiwa"

"Ni muhimu kusimama tena na kuendelea kupambana baada ya kuanguka , usikate tamaa. Naipenda timu yangu ya Yanga, nitaiunga mkono na kuipigania," aliandika Molinga kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Mcongomani huyo jioni ya leo, saa moja anatarajiwa kukiongoza kikosi cha Yanga katika mchezo dhidi ya Singida United, mchezo ambao mabingwa hao wa kihistoria wanahitaji ushindi ili kupoza 'machungu' ya kupoteza mchezo uliopita kwa kufungwa mabao 4-1 na Simba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’