Kiungo fundi wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto' ataukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida United utakaopigwa kesho Jumatano kwenye uwanja wa Taifa akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano
Tangu arudishwe kwenye kikosi cha kwanza na kocha Luc Eymael, Fei Toto amekuwa 'injini' ya safu ya kiungo ya Yanga akishirikiana vyema na Mnyarwanda Haruna Niyonzima
Katika mchezo dhidi ya Simba, Fei Toto ndiye aliyekuwa nyota miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao kwa hakika walitetereka na kujikuta wakibugizwa mabao 4-1 na watani zao
Kadi ya njano aliyopata katika mchezo huo itamfanya abakie jukwaa wakati Yanga ikihitaji ushindi dhidi ya Singida United ili kuweka hai matumaini ya kumaliza kwenye nafasi ya pili
Lakini pia Yanga itawakosa nahodha msaidizi Juma Abdul na beki Said Juma Makapu ambao pia wana kadi tatu za njano
Mkongwe Kelvin Yondani huenda akarejeshwa katika nafasi yake ya ulinzi katika mchezo huo, wakati Abdulaziz Makame 'Bui' anaweza kuchukua nafasi ya Fei Toto huku Deus Kaseke akirejea kwenye majukumu ya safu ya ulinzi wa kulia