Makambo ni suala la muda Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jul 2020
Makambo ni suala la muda Yanga

Juzi mashabiki wa Yanga walipatwa na huzuni kubwa baada ya kuishuhuda timu yao ikichapwa mabao 4-1 na watani zao Simba katika mchezo wa nusu fainali kombe la FA

Suala la kipigo lilikuwa jambo moja, lakini kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji ni jambo jingine lililokatisha tamaa na wengi kuona ulazima wa kufanyika maboresho makubwa katika kikosi cha timu hiyo kuelekea msimu ujao

Habari njema ni kuwa tayari michakato ya maboresho ya Yanga ilishaanza mapema hesabu zikiwa kutwaa ubingwa msimu ujao

Yanga tayari imeshanasa sahihi za wachezaji wawili kulingana na chanzo kisicho na shaka ndani ya uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria

Hawa ni winga Tuisila Kisinda kutoka AS Vita na beki wa kushoto Erick Rutanga huku mabingwa hao wa kihistoria wakiwa kwenye hatua za mwisho kumalizana na washambuliaji wengine wawili

Imefahamika mmoja wa washambuliaji hao ni Heritier Makambo, nyota wa zamani wa mabingwa hao wa kihistoria ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Horoya AC ya Guinea

Awali Yanga ilipiga hodi Horoya ikimuhitaji mchezaji huyo kwa mkopo, Horoya 'wakachomoa' lakini wakawa tayari kumuuza moja kwa moja

Makambo bado ana mkataba wa miaka miwili na Horoya AC, anaweza kuigharimu Yanga sio chini ya Tsh Milioni 200 kuweza kumnasa

Jambo la uhakika ni kuwa msimu ujao safu ya ushambuliaji ya Yanga itaundwa na sura mpya za kazi

Aidha matokeo dhidi ya Simba juzi yamewatia hasira mabosi Yanga na wadhamini wao GSM ambao sasa wanapasua anga kukamilisha michakato yote ya usajili iliyokuwa ikisubiri ligi kufika mwishoni

Pamoja na Makambo, Mbukinarbe Yacouba Sogne na Mcongomani Mpiana Monzizi mmoja wao au wote wanaweza kuibukia Jangwani

Kulingana na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, nyota watano wa kigeni wanaweza kusajiliwa huku idadi kama hiyo ikitarajiwa kwa upande wa wazawa

Ndani ya wiki mbili vifaa vipya vitaanza kutambulishwa rasmi pale Jangwani kuelekea tukio kubwa la wiki ya Mwananchi ambalo awamu hii litakuwa tofauti kabisa

Safari hii Yanga haitaweka kambi kule Morogoro kama ilivyokuwa msimu uliopita, kocha Luc Eymael anaweza kwenda kuwaandaa vijana wake Afrika Kusini au Ubelgiji

Inafahamika maandalizi hafifu mwanzoni mwa msimu ni moja ya sababu zilizopelekea Yanga kukosa muunganiko tangu mwanzo wa msimu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’