Yanga kupoza machungu kwa Singida United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jul 2020
Yanga kupoza machungu kwa Singida United

Baada ya kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa watani zao Simba hapo jana, kikosi cha Yanga kimerudi kujipanga kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida United ambao utapigwa keshokutwa Jumatano katika uwanja wa Taifa

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema wamesahau matokeo ya mchezo wa jana na sasa wanajipanga kuikabili Singida United

Yanga imebaki na vita moja tu ya kuwania nafasi ya pili baada ya kipigo cha Simba kuwaondoa kwenye michuano ya kombe la FA

Mabingwa hao wa kihistoria wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Azam Fc na Namungo ambazo pia zinawania nafasi hiyo

Wanakutana na Singida United ambayo tayari imejihakikishia kuteremka daraja

Pengine huu ndio mchezo ambao Yanga wanaweza kuutumia kurudisha kujiamini kwa wachezaji wake

Hata hivyo wachezaji wanapaswa kusahau matokeo ya mchezo wa jana waweze kufanya vizuri kwenye mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’