Lazima tukubali, tunapaswa kuimarisha timu tuweze kuwa na uhalali wa kushindana Simba, kwani wao wako mbali sana, ukiangalia mpira wanaocheza, wameiva
Nadhani Simba wamestahili kupata ushindi mnono, kikosi chao kimeonyesha kuwa bora kama timu na hata kwa mchezaji mmoja mmoja
Njia moja ya kujiimarisha ni kukubali kushindwa kisha kufanyia kazi mapungufu yako
Baada ya kushindwa kushiriki michuano ya Kimataifa kwa takribani misimu minne mfululizo, Simba walikaa chini kujibu maswali ya nini kilichokuwa kikiwakwamisha
Nadhani jambo hili linapaswa kufanywa na Yanga pia
Mashabiki wa Yanga hawajazoea machungu haya wanayopita sasa, pengine ni kutokana na mafanikio mfululizo ambayo timu imekuwa ikipata
Hata hivyo, matokeo haya ni sawa na sindano anayochomwa mgonjwa. Inauma lakini ndani yake kuna tiba
Ni wazi viongozi wa Yanga pamoja na wadhamini wanapaswa kukaa chini kuweka mpango mkakati wa kuirudisha Yanga pale palipozoeleka na sio kuja na majibu ya muda mfupi ambayo hayawezi kuwa na manufaa huko mbeleni