Kikosi cha Yanga jioni ya leo kitashuka kwenye uwanja wa Taifa kuumana na watani zao Simba katika mchezo wa nusu fainali michuano ya kombe la FA (ASFC)
Ni mchezo ambao Yanga inahitaji kushinda ili kutinga fainali ya michuano hiyo
Hakika ni moja ya michezo muhimu ambayo Yanga imecheza msimu huu. Kwani hatma ya ushiriki katika michuano ya Kimataifa msimu ujao, itaanza kuamuliwa na matokeo ya leo
Yanga iliweka kambi ya siku mbili mkoani Kagera baada ya mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar ambao walishinda kwa bao 1-0
Walirejea jijini Dar es salaam juzi na jana wakakamilisha maandalizi yao ya mwisho
Mkufunzi wa Yanga Luc Eymael amesema vijana wake wako tayari kuwakabili watani zao Simba katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali
Mchezo utapigwa kuanzia mishale ya saa 11 jioni ukitarajiwa kuhudhuriwa na mashabiki 30,000
Kila la kheri Yanga, kila la kheri mabingwa wa kihistoria
Β
Β