Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeweka hadharani majina ya waamuzi sita ambao watachezesha mchezo wa nusu fainali kombe la FA kati ya Simba dhidi ya Yanga ambao utapigwa keshokutwa Jumapili, Julai 12 kwenye uwanja wa Taifa
Mwamuzi wa kati atakuwa Abubakar Mturo kutoka mkoani Mtwara ambaye atasaidiwa na Abdallah Mwinyikuu (Singida) na Nadeem Alloyce (Dar)
Waamuzi wengine wa ziada ni Ramadhani Kayoko (Dar), Frank Kombe (Dar) na Kassim Mpanga (Dar)
Muda wa mchezo ni saa 11 jioni

ADVERTISE HERE