Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amemsifu mlinda lango Farouk Shikhalo kwa kuonyesha kiwango kizuri kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao uliishuhudia Yanga ikiondoka na ushindi wa bao 1-0
Eymael amesema Shikhalo alikuwa nyota wa mchezo huo akiisaidia Yanga kuondoka na ushindi muhimu
"Nampongeza Shikhalo, alikuwa na mchezo mzuri sana. Aliokoa mashambulizi ya hatari kwenye kipindi cha kwanza na akafanya hivyo katika kipindi cha pili. Hakika anastahili pongezi," alisema Eymael
Eymael alimuanzisha Shikhalo kwenye mchezo huo akichukua nafasi ya Metacha Mnata ambaye kwa mechi za karibuni amejihakikisha nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Hata hivyo Shikhalo ameanza kurejesha makali yake, pengine Eymael atakuwa na wakati mgumu kuchagua nani aanze kwenye mchezo dhidi ya Simba