Morrison amerudi, kazi wanayo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jul 2020
Morrison amerudi, kazi wanayo

Winga Bernard Morrison leo amewapa furaha mashabiki wa Yanga baada ya kufunga bao pekee lililowahakikishia ushindi mabingwa hao wa kihistoria kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Kagera SugarΒ  ambao ulipigwa uwanja wa Kaitaba

Morrison alikosekana kwenye kikosi cha Yanga kwa wiki kadhaa baada ya kuibua sintofahamu kuhusu mkataba wake, hali iliyopelekea suala lake kuamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)

Morrison amedhihirisha umuhimu wake leo mbele ya Kagera Sugar, pamoja na kufunga bao la ushindi, kwa muda mwingi aliwaweka kwenye presha walinzi wa Kagera Sugar ambao walishindwa kumdhibiti

Hakuna shaka Morrison atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoikabili Simba Jumapili ya Julai 12 2020 katika mchezo wa nusu fainali kombe la FA

Pamoja na ushindi wa leo, Yanga inakwenda kuumana na Simba wachezaji wakiwa na ari kubwa pamoja na uwepo wa Morrison ambaye amedhihirisha ni mchezaji anayeweza kufanya jambo wakati wowote anapokuwa uwanjani

Pengine sasa unaweza kuelewa kwa nini wakati nyota huyo alipokuwa na mgogoro na viongozi wake, baadhi ya mashabiki wa Simba walikuwa wakifurahia hali hiyo wakiamini atakosekana Julai 12

Nyota huyo ndiye anayehofiwa zaidi na Simba kwenye kikosi cha Yanga kwani alipeleka kilio Msimbazi katika mchezo wa mwisho ambao timu hizo zilikutana uwanja wa Taifa na Yanga kuondoka na ushindi wa bao 1-0

Mwamba huyu atakuwepo tena uwanja wa Taifa, Julai 12...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’