Ngasa aahidi 'kuwashughulikia' Kagera Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jul 2020
Ngasa aahidi 'kuwashughulikia' Kagera Sugar

Jioni ya leo kikosi cha Yanga kitashuka kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba kuumana na Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Timu hizo zinakutana ikiwa ni wiki moja imepita baada ya kuchuana vikali kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA ambao ulipigwa jijini Dar es salaam na Yanga kutinga nusu fainali ya michuano hiyo kwa ushindi wa mabao 2-1

Winga mkongwe Mrisho Ngasa ndiye aliyekuwa chachu ya ushindi wa Yanga katika mchezo huo

Alimtengenezea nafasi David Molinga kuweka kambani bao la kusawazisha kabla ya kusababisha mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na Deus Kaseke na kuihakikishia Ynga ushindi muhimu

Kuelekea mchezo wa leo, Ngasa amesema wachezaji wako tayari kuikabili Kagera Sugar katika mchezo ambao wanafahamu hautakuwa mwepesi

"Sisi tuko tayari, tunajua hautakuwa mchezo rahisi lakini tunawaambia mashabiki wetu, tutaendeleza pale tulipoishia kwenye mchezo uliopita hivyo waje kwa wingi uwanjani," alisema Ngasa

Ngasa amekuwa na mwendelezo mzuri tangu ligi iliporejea baada ya mapumziko na corona

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’