Kuelekea mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili Julai 12 katika uwanja wa Taifa, wadhamini na wasambazi wa jezi za klabu ya Yanga, GSM wametoa ofa ya punguzo la bei ya jezi hadi Tsh 15,000/-
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema ofa hiyo itadumu kwa muda wa mwezi mmoja hivyo kuwataka wapenzi, mashabiki na wanachama wa Yanga kuchangamkia fursa hiyo
Jezi hizo zinapatikana katika maduka yote ya GSM nchini
Hii ni nafasi kwa Mwanayanga 'kutokelezea' ndani ya uzi wa mabingwa wa kihistoria kwenye mchezo dhidi ya Simba hapo Jumapili
ADVERTISE HERE