Kagera Sugar vs Yanga, mechi ya kibabe Kaitaba leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jul 2020
Kagera Sugar vs Yanga, mechi ya kibabe Kaitaba leo

Kikosi cha Yanga jioni ya leo kitashuka dimba la Kaitaba Bukoba kuumana na Kagera Sugar katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali

Msimu huu Kagera Sugar ni miongoni mwa timu zilizoipa Yanga changamoto katika michezo miwili waliyokutana kila timu ikishinda mchezo mmoja

Kagera Sugar ilishinda mchezo wa kwanza wa ligi kwa mabao 3-0 na Yanga ikashinda mchezo wa robo fainali kombe la FA kwa mabao 2-1

Kwa Kagera Sugar, mechi ya leo wanaichukulia kama mechi ya kisasi wakiwa na kumbukumbu ya kutupwa nje kombe la FA

Kwa upande wa Yanga, mchezo wa leo utakuwa maandalizi muhimu kuelekea mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya watani zao Simba

Pamoja na kuwa mabingwa hao wa kihistoria watachukua tahadhari kuepuka kadi na majeruhi, hawatauchukulia 'poa' mchezo huu hasa ikizingatiwa wanahitaji kumaliza katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi

Kiungo Haruna Niyonzima na nahodha Msaidizi Juma Abdul huenda wasiwepo kwenye kikosi kitakachoshuka dimbani leo kutokana na majeruhi

Hata hivyo winga Bernard Morrison yuko 'fit', anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji leo, akinoa makali kuelekea mchezo dhidi ya Simba

Takwimu zinaibeba Yanga kuelekea mchezo huo ambao unapigwa katika uwanja wa Kaitaba kwani katika kipindi cha angalau misimu mitatu iliyopita, wameshinda mechi zote walizocheza katika uwanja huo

Baada ya mchezo huo kikosi cha Yanga kitakwea pipa usiku wa leo kurejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’