Kiungo wa Yanga Mohammed Issa 'Banka' aliwasili mkoani Kagera mapema leo na ameshiriki mazoezi ya mwisho ya Yanga kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Kaitaba
Yanga imekamilisha maandalizi yake ya mwisho tayari kwa mtanange huo unaosubiriwa kwa hamu
Banka aliyekosekana kikosini kwa wiki kadhaa, alijumuika na wachezaji wenzake katika maandalizi hayo ya mwisho

Katika hatua nyingine, wachezaji Haruna Niyonzima na Juma Abdul wao walipewa program maalum wakati wachezaji wengine wakiendelea na mazoezi
Ni wazi nyota hao huenda wasiwe sehemu ya kikosi kitakachoikabili Kagera Sugar kesho
Niyonzima na Abdul walikuwa miongoni mwa nyota sita wa Yanga waliopata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Biashara United juzi
Habari njema kwa Yanga ni kuwa ukiondoa Niyonzima na Abdul, wachezaji wengine wote wako tayari kwa mchezo huo