Kikosi cha Yanga leo kinakamilisha maandalizi ya mwisho uwanja wa Kaitaba kabla ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa kesho Jumatano
Mabingwa hao wa kihistoria walitua Bukoba mapema jana na kuanza kujifua jioni tayari kwa mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wakazi wa Kagera na maeneo ya jirani
Ni mchezo muhimu kwa Yanga katika mapambano ya kuwania nafasi ya pili
Lakini pia ni mchezo ambao mabingwa hao wa kihistoria watapaswa kuwa na tahadhari kubwa kujiepusha na kadi, majeruhi kuelekea mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili
ADVERTISE HERE