Mkongwe na nyota aliyejijengea ufalme katika klabu ya Yanga miaka ya sabini Kitwana Manara 'Computer' leo alitembelea Banda la klabu ya Yanga kwenye maonesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba
Legendari huyo alipata nafasi ya kupiga picha na Mashabiki wanaoendelea kumiminika kwenye banda la Yanga kujipatia huduma mbalimbali
Manara pia amewasilisha picha za kikosi cha Yanga miaka ya 70 akikusanya fedha kwa ajili ya kumsaidia nyota mwingine wa zamani Jellah Mtagwa ambaye ni mgonjwa

Yanga imeziweka picha hizo kwenye banda lake na zinapatikana kwa Tsh 3,000/- kulingana na Afisa habari wa timu hiyo, Hassan Bumbuli
Mzee Manara ni Baba mzazi wa Msemaji wa Simba Haji Manara
ADVERTISE HERE