Uwanja wa Karume 'wamchefua' Eymael

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jul 2020
Uwanja wa Karume 'wamchefua' Eymael

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael ameeleza kushangazwa na mamlaka za usimamizi wa soka nchini kuruhusu matumizi ya uwanja wa Karume unaotumiwa na Biashara United

Akizungumza baada ya timu yake kulazimishwa sare tasa dhidi ya Biashara United, Eymael alisema uwanja huo hauna hadhi ya kutumika kwa ajili ya mpira wa miguu

"Ni aibu kwa timu kubwa kama Yanga kucheza katika uwanja huu ambao hadhi yake ni ya kuchungia mifugo, vyumba vya kabadilisha nguo havifai, inashangaza kuona wasimamizi wa mpira wanaruhusu uwanja huu kuendelea kutumika," alisema Eymael

"Mimi nawafundisha wachezaji wangu kucheza kandanda safi la burudani, lakini haiwezekani kucheza katika kiwanja kama hiki. Nawapongeza wachezaji wangu wamepambana, tumekosa bahati tu"

Aidha Eymael amesema matokeo hayo yamemvurugia mipango yake lakini wataendelea kupambana mpaka mwisho kuhakikisha wanatimiza malengo ya kumaliza katika nafasi ya pili

Azam Fc iliipiku Yanga kwenye nafasi ya pili baada ya kuifumua Singida United mabao 7-0. Yanga itacheza na Singida United baada ya mchezo wao wa kombe la FA dhidi ya Simba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’