Hongera Mkwassa, Jembe la Yanga

Admin By Admin
β€’
1 Jul 2017
Hongera Mkwassa, Jembe la Yanga
Kwa namna ya kipekee tunampongeza Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwassa kwa ushupavu wake ambao umepelekea amani ya mashabiki wa Yanga kurejea.

Msimu uliomalizika ulikuwa mgumu sana hasa baada ya Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji kukumbwa na matatizo ambayo kila mtu anayafahamu.

Ilifika kipindi klabu ilikosa mwelekeo kwani hata mishahara ya wachezaji haikuwepo.

Lakini busara ya Mkwassa na viongozi wenzake walifanikisha timu kuendelea kupambana hadi kufanikiwa kutwaa ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo licha ya matatizo lukuki.

Aidha chini ya uongozi wake Yanga imefanikiwa kupata udhamini wa karibu Bil 1 kwa mwaka kutoka kampuni ya SportPesa.

Pia tunamshuhudia sasa akiivusha Yanga katika kipindi kingine kigumu cha usajili.

Ilifika kipindi kila mtu alikata tamaa baada ya ukimya wa muda mrefu. Wapinzani wa Yanga walitumia mwanya huo kunena mambo ya uongo lakini Katibu Mkuu alisisitiza Yanga itavuka salama mashabiki wasipate taharuki.

Leo hii Yanga imefanikiwa kuwabakisha wachezaji wake muhimu ukiondoa Niyonzima aliyetaka kuifilisi Yanga pamoja na kusajili wachezaji wazuri.

Kwa wale wasiofahamu Mkwassa ndiye aliyeachiwa jukumu la kusimamia usajili na kocha George Lwandamina.

Lwandamina aliacha vigezo tu vya wachezaji anaowataka. Hii ni kwa sababu alitambua Mkwassa ni kocha tena wa kiwango cha juu.

Hivyo msidhani Yanga imesajili magalasa, wachezaji wote waliosajiliwa Yanga wanasifa za kuitumikia Yanga na kuipa mafanikio.

Naiona Yanga imara sana mikononi mwa Katibu Mkuu Charles Mkwassa. Msimu ujao 2017-18 unaweza ukawa wa furaha sana kwa mashabiki wa Yanga hasa katika michuano ya Kimataifa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’