Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi na winga Beranrd Morrison hawakujumuishwa kwenye kikosi kilichoelekea kanda ya ziwa kwa ajili ya michezo dhidi ya Biashara United na Kagera Sugar
Tshishimbi alianza mazoezi mapema wiki hii. Mcongomani huyo ameachwa aimarike zaidi tayari kuwakabili Simba kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la FA, Julai 12
Morrison alirejeshwa kikosini juzi baada ya mvutano na mabosi wake Yanga kufikia tamati. Hata hivyo kocha Luc Eymael alimuondoa mapema tu kwenye kikosi chake ambacho kiko Musoma kwa kuwa hakuwa amefanya mazoezi na timu siku kadhaa nyuma
Hata hivyo Eymael alisema Morrison anaweza kuungana nao mkoani Kagera kama ataona kuna umuhimu kumtumia mchezo dhidi ya Kagera Sugar
Lakini amewahakikishia Wanajangwani kuwa Morrison atakuwa sehemu ya kikosi chake kitakachoikabili Simba Julai 12