Ndivyo unavyoweza kusema baada ya winga Bernard Morrison kuibuka mazoezini leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Biashara United na Kagera Sugar bila kusahau mchezo wa kombe la FA dhidi ya Simba ambao utapigwa Julai 12
Morrison alikuwa kwenye mvutano na uongozi wa Yanga kuhusiana na suala la mkataba lakini pia ni madai ya Yanga kuwa klabu ya Simba imekuwa ikimvuruga nyota huyo aondoke Jangwani
Yanga ilifungua kesi TFF na bado suala hilo linaendelea kushughulikiwa
Morrison ni mchezaji muhimu kuelekea mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Simba
Bila shaka mwamba huyu atakuwepo Julai 12 kuwanyoosha


ADVERTISE HERE