Lile tukio kubwa la utambulisho wa timu kuelekea msimu mpya tayari linakaribia ambapo uongozi wa Yanga umewaweka sawa mashabiki wake
Iko hivi, Yanga imedhamiria kufanya mambo makubwa na zaidi ni utambulisho wa nyota wapya ambapo inaelezwa usajili wa wachezaji wapya umekamilika kwa asilimia 90 kinachosubiriwa ni wakati mwafaka tu mambo kuwekwa hadharani
Lakini pia GSM wako jikoni 'wakipika' uzi mpya wa Yanga kwa ajili ya msimu ujao
Inaelezwa uzi huo utakuwa bora mara dufu ya uzi wa msimu huu
Hatari zaidi ni siku ya kilele cha tukio lenyewe, kuna timu kubwa kutoka kule Hispania inaweza kutua nchini
Hakika msimu ujao, furaha na shamrashamra zitarejea Jangwani
ADVERTISE HERE