Ni rasmi mchezo wa nusu fainali kombe la shirikisho la Azam (ASFC) utazikutanisha Yanga na Simba baada ya matokeo ya mchezo wa leo kati ya Simba dhidi ya Azam uliomalizika kwa Simba kupata ushindi wa mabao 2-0
Huu utakuwa mchezo wa tatu kwa Yanga na Simba kukutana msimu huu, Yanga ikitoka kidedea katika michezo miwili iliyopita kwa kupata ushindi na matokeo ya sare
Yanga sasa itakuwa na kazi moja tu, kumaliza mnyama ili kujihakikishia nafasi ya kucheza fainali
Utakuwa mchezo mkali na wenye ushindani kutokana na historia ya timu hizi kongwe zaidi nchini
Timu zilizotinga hatua ya nusu fainali baada ya matokeo ya mechi za leo ni Namungo, Yanga, Sahare All Stars na Simba
Nusu fainali ya kwanza ni kati ya Namungo dhidi ya Sahare na nusu fainali ya pili ni kati ya Yanga dhidi ya Simba