Mshambuliaji Mcongomani David Molinga 'Falcao' ameanza kuonyesha makali yake wakati ligi ikielekea ukingoni
Katika mechi tatu zilizopita, Molinga amefunga mabao matatu huku akiwa chachu ya ushindi dhidi ya Kagera Sugar na kuisaidia Yanga kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la FA
Katika mchezo huo uliopigwa jana Jumanne kwenye uwanja wa Taifa, Molinga alifunga bao la kwanza na pasi yake murua ilipelekea Mrisho Ngasa kufanyiwa madhambi yaliyoipa Yanga pigo la mkwaju wa penati ambao uliwekwa kambani na Deus Kaseke
Molinga sasa amefunga mabao 10 kwenye ligi na mabao mawili kwenye michuano ya kombe la FA hivyo kufikisha mabao 12
Mkataba wake na Yanga unamalizika mwezi wa nane na tayari kuna taarifa kuwa huenda akajiunga na RS Bekane, miamba wa soka nchini Morocco
Hata hivyo Molinga mwenyewe amesema anawasikilizia Yanga kama watampa ofa nono ili aendelee kubaki
Inaelezwa mechi zilizobaki kumalizia msimu ndizo zitakazoamua kama Molinga anaweza kuongezwa mkataba au la
Wanajangwani mnasemaje, abaki au aletwe mbadala?