Pamoja na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar, hakika lazima tukiri Yanga leo haikuwa na mchezo mzuri kabisa mbele ya Kagera Sugar
Ni wazi kocha Luc Eymael hakumsoma vizuri mpinzani wake Meckie Mexime kwani alikuja na mbinu zilezile alizotumia kupata ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wa ligi
Mexime ameonyesha kubaini mbinu za Eymael na hivyo kumpa wakati mgumu katika muda wote wa mchezo huo
Kama ulivyokuwa mchezo wa ligi, Kagera Sugar walikuwa bora, Yanga walilazimika kujihami zaidi na kutumia mashambulizi ya kushitukiza
Kagera Sugar walicheza 'toto football', walijilinda pamoja na kwenda kushambulia pamoja
Kagera Sugar walihakikisha wanakuwa na namba kubwa zaidi ya washambuliaji wa Yanga pale wanapojilinda na pia kuwa na namba kubwa zaidi ya walinzi wa Yanga pale waliposhambulia
Ni wazi Mkufunzi wa Yanga Luc Eymael ana kazi ya kufanya ili kikosi chake kifanikiwe kutinga fainali na hata kutwaa ubingwa
Ikumbukwe Yanga itakutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba dhidi ya Azam Fc
Mchezo huo pengine ndio utakaokuwa fainali ya michuano hii, kwani timu itakayoshinda itakuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa