Kiungo mahiri wa Mtibwa Sugar, Mohamed Issa 'Banka' amesema mkataba wake na klabu hiyo uko ukingoni na yuko tayari kujiunga na timu yoyote atakayofikia nayo makubaliano.
Kiungo huyo aliyejiunga na Mtibwa mwaka jana amekuwa gumzo baada ya kuonyesha umahiri kwenye michezo tisa aliyocheza kwenye kikosi cha Mtibwa kwenye ligi kuu ya Vodacom.
Yanga ni miongoni mwa timu zinazomnyemelea Banka.
"Nakaribia kumaliza mkataba wangu na Mtibwa hivi karibuni ila siwezi kusema ni lini na sijajua kama nitaongeza ama nitabaki," amefunguka Banka
"Mimi ni mchezaji nipo tayari kwenda timu yeyote inayonihitaji ijapokuwa siwezi sema ni timu gani zimenifuata hadi sasa kwa kuwa sihitaji kuweka wazi kila kitu hadi kikamilike lakini ieleweke kuwa kuna timu zinanitaka na siyo moja."
Dirisha la usajili limefunguliwa rasmi leo Novemba 15 likitarajiwa kufungwa Disemba 15

ADVERTISE HERE