Kiungo wa Yanga Mapinduzi Balama amewashukuru wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kwa kumtakia kheri aweze kupona majeraha aliyopata hivi karibuni
Mapinduzi aliumia kifundo cha mguu kwenye mazoezi ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ndanda Fc
"Ninafarijika kuona wengi wameguswa na kunitakia kheri niweze kupona haraka. Ni upendo mkubwa sana ambao wenzangu wamenionyesha. Nawashukuru wachezaji wenzangu bila ya kuwasahau mashabiki wote," alisema
Balama anatarajiwa kuwa nje kwa wiki tatu akiuguza majeraha hayo. Ni wazi hataweza kucheza mechi zilizobaki kukamilisha msimu huu
ADVERTISE HERE