Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kufika tamati Julai 26 tayari kuanza maandalizi ya msimu mpya
Ugonjwa wa corona umevuruga mipango ya msimu huu ambapo baada ya ligi kumalizika timu zitakuwa na muda mdogo wa mapumziko kabla ya kuanza msimu mpya
Dirisha la usajili litafunguliwa August 01 na litafungwa August 31
Mabingwa wa kihistoria Yanga wao wameanza mapema michakato ya usajili wakiwa katika mkakati kabambe wa kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao
Hivi karibuni Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alifichua kuwa wanaendelea na michakato ya usajili na wataanza kuweka hadharani 'vifaa' baada ya msimu kufika tamati
Yanga imedhamiria kufanya tukio kubwa la utambulisho wa kikosi katika hafla ya wiki ya Mwananchi
Antonio Nugaz ambaye ni Afisa Mhamasishaji amesema safari hii wiki ya Mwananchi itaacha historia