Ukizungumzia wachezaji wanaofanya vizuri sana kwenye kikosi cha Yanga wakati huu, huwezi kukosa kutaja jina la winga Deus Kaseke 'Deda 27'
Tangu kurejea kwa ligi baada ya janga la corona, kiwango cha Kaseke kimeonekana kuimarika, hakika ni mtu muhimu sana kwenye kikosi cha Yanga wakati huu
Kaseke anaibeba Yanga, mabao yake mawili aliyofunga dhidi ya Ndanda Fc jana, yanadhihirisha umuhimu wake kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria
Msimu huu Kaseke amehusika kutoa pasi tano za mabao, akishirikiana vizuri na Juma Abdul ambaye jana aliongeza 'assist' zake kufika 7
cutKazi yake uwanjani inaonekana, huyu anastahili kupewa mkataba mpya kuendelea kukipiga Jangwani
Kwani mkataba wake utamalizika mwezi ujao. Ameonyesha ni mchezaji anayestahili kupewa mkataba mpya
Mabao yake mawili aliyofunga jana, huenda yakampa sababu kocha Luc Eymael kumtumia kama mshambuliaji wa kati mechi zijazo