Baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ndanda Fc hapo jana, keshokutwa Jumanne, kikosi cha Yanga kitarejea uwanja wa Taifa kuikabili Kagera Sugar ukiwa ni mchezo wa robo fainali michuano ya kombe la FA (ASFC)
Tayari ubingwa unaelekea upande wa pili, hii ndio michuano ambayo Yanga imebaki na matumaini ya kushiriki mashindano ya CAF msimu ujao
Hakuna kingine zaidi ya ushindi na kufanikiwa kutinga nusu fainali kuwasubiri Simba au Azam Fc
Habari njema kwa mabingwa hao wa kihistoria ni kurejea kwa winga Bernard Morrison ambaye amemaliza adhabu ya kukosa mechi mbili
Pamoja na kuwa hivi karibuni Morrison aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa Yanga, lakini baada ya kufanya kikao pamoja na mabosi wake ambacho pia kiliwajumuisha wachezaji wote, nyota huyo raia wa Ghana aliahidi kuipigania timu kuhakikisha inafikia malengo yake
cutLakini pia beki kisiki Lamine Moro, amemaliza adhabu ya mechi tatu nae atakuwa tayari kuelekea mchezo
Nahodha Papy Tshishimbi atafanyiwa vipimo vya afya kubaini utimamu wake kuelekea mchezo huo
Ni mchezo ambao Yanga inahitaji silaha zote ili kusonga mbele hatua inayofuata
Kwa kocha Luc Eymael, huu ni mchezo muhimu wa kisasi. Ni hawahawa Kagera Sugar walimkaribisha Tanzania kwenye ligi kuu kwa kipigo cha mabao 3-0
Lakini wakati huu watakutana na Yanga tofauti ambayo imeiva