Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kuwa kiungo wake mshambuliaji Mapinduzi Balama atakuwa nje kwa wiki tatu baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu kweye mazoezi ya timu hiyo jana
Balama tayari amepatiwa matibabu ambapo mguu wake umefungwa bandeji gumu (P.O.P) itakayomsaidia kuurejesha katika hali ya kawaida
Jana hofu ilikuwa kubwa, kwani mguu wake ulionekana kupinda kabla ya kufanyiwa uchunguzi wa kina na madaktari kuthibitisha kuwa yuko salama na atakaa nje kwa wiki tatu
Balama huenda akakosa mechi zilizobaki kumaliza msimu, akianzia na mchezo wa leo dhidi ya Ndanda Fc
ADVERTISE HERE