Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amefichua kuwa mchakato wa usajili uko vizuri mpaka sasa wakiwa wamemalizana na wachezaji watano
Bila ya kutaja majina ya wachezaji hao, Hersi amesema miongoni mwao, watatu ni nyota wa kigeni na wawili ni wazawa
Kati ya hao nyota watatu wa kigeni, mmoja ni winga na mwingine ni beki
Aidha Hersi amesema pia wako katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa nyota wengine wawili wa kigeni
"Tumeweka mkazo kwenye usajili kuhakikisha msimu ujao tunakuwa na timu ya kutwaa ubingwa. Mpaka sasa tayari tumemalizana na wachezaji kama watano, watatu kutoka nje ya nchi na wawili wazawa"
"Wachezaji wengine wawili kutoka nje ya nchi tuko mbioni kumalizana nao pia. Kama isingekuwa changamoto ya corona, tungekuwa tumekamilisha kila kitu," alisema Hersi
Miongoni mwa nyota wa kigeni ambao wanatajwa kuwa usajili wao umekamilika ni winga Tuisila Kisinda kutoka AS Vita na beki Erick Rutanga kutoka Rayon Sport
Aidha Mhandisi Hersi amesema watafanya usajili kabambe akiwahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa mpango wa usajili uliopo ni bab-kubwa
Yanga huenda ikaongeza nyota watano wa kigeni na kuachana na wengine watano
Wachezaji wa kigeni ambao wana nafasi kubwa ya kubaki Yanga ni pamoja na Farouk Shikhalo, Lamine Moro, Papy Tshishimbi, Bernard Morrison na fundi mwenyewe Haruna Niyonzima 'Fabregas'