Kikosi cha Yanga jioni ya leo kitashuka uwanja wa Taifa kuikabili Ndanda Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Baada ya kukosa ushindi katika michezo mitatu iliyopita, mchezo huu ni wa kufa na kupona kwa mabingwa hao wa kihistoria
Kocha Mkuu Luc Eymael amesema vijana wake wako tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao ushindi utaweka hai matumaini ya kumaliza ligi katika nafasi ya pili
Lakini pia kama Yanga haitashinda, na Azam ambao watakuwa Mara nao wakakosa ushindi, basi Simba itaondoka na ubingwa bila ya kushuka uwanjani, mechi yao na Prisons imepangwa kesho Jumapili
Viingilio vya mchezo huo unaopigwa saa kumi jionii, VIP ni Tsh 15,000/- VIP B na C ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Hizi hapa mechi zote zinazopigwa leo Jumamosi;

ADVERTISE HERE