Nyota Yanga wamjadili Morrison

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Jun 2020
Nyota Yanga wamjadili Morrison

Jana wachezaji wa klabu ya Yanga walifanya kikao ambacho kiliwashirikishia viongozi wao wa benchi la ufundi

Kikao hicho kilikuwa maalum kuweka sawa mikakati ili kuhakikisha wanafanya vizuri mechi zilizobaki kufuatia mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha

Lakini pia nyota hao walitumia kikao hicho kumjadili winga Bernard Morrison ambaye hivi karibuni aliingia katika mgogoro na uongozi wa Yanga baada ya kuibua sintofahamu kuhusu mkataba wake

Wachezaji wa Yanga walionyesha wasiwasi kutokana na kauli zake alizotoa katika mahojiano na Mwandishi Saleh Ally Jembe na walimtaka kuwahakikishia kama yuko nao

Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul amesema walihitaji kusikia msimamo wake ili wasije wakamuweka katika mikakati yao kumbe yeye hayupo nao

"Tulitaka atueleze wazi kama tuko pamoja au tusimuhesabu kwenye programu zetu. Tunajua ana mgogoro wake na uongozi lakini huu hautuhusu katika kuipigania timu, ilikuwa muhimu tujue msimamo wake ndani ya timu kama tuko pamoja naye isije kuwa sisi tunamipango yetu naye ana mambo yake," Abdul aliiambia tovuti ya Yanga

Morrison amewatoa hofu wachezaji wenzake akiahidi kuipigania timu kuhakikisha inafikia malengo yake

Juzi Morrison aliingia matatani baada ya kudai kuwa hana uhakika kama ataendelea kubaki Yanga baada ya mkataba wake wa miezi sita utakapomalizika Julai 14 huku akisema kuwa hakusaini mkataba mpya na mabingwa hao wa kihistoria

Hata hivyo uongozi wa Yanga kupitia taarifa ya Kaimu Katibu Mkuu, ulijitokeza hadharani na kubainisha kuwa nyota huyo raia wa Ghana alisaini mkataba wa miaka miwili March 20 2020, mkataba ambao utaanza baada ya ule wa awali kumalizika Julai 14

Uongozi wa Yanga uliwahakikishia mashabiki na wanachama wake kuwa mkataba wake ulisajiliwa TFF na FIFA hivyo hakuna shaka kuhusu hatma yake

Aidha kwa kitendo cha kufanya mahojiano na chombo cha habari wakati akiwa kambini, Morrison alipigwa faini ya Tsh Mil 1.5

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’