Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amefichua kuwa baada ya mabingwa hao wa kihistoria kufanikiwa kumnasa mlinzi wa kushoto wa Rayon Sport Erick Rutanga, mlinzi mwingine wa kati anatarajiwa kusajiliwa
Eymael amesema anahitaji mchezaji ambaye atamudu vyema nafasi ya beki wa kati ambaye ataongeza nguvu kwenye kikosi chake
"Tunahitaji kuongeza beki mwingine wa kati ambaye ataingia moja kwa moja kwenye timu na kuboresha eneo hilo ambalo mara nyingi tunamtumia Said Juma Makapu licha ya kuwa sio eneo lake asilia"
"Nafurahi kuona viongozi wanafanyia kazi mapendekezo yangu kwenye usajili, msimu ujao nadhani tutakuwa na timu imara," alisema Eymael
Yanga imekuwa ikihusishwa na mlinzi wa Coastal Union Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye habari za uhakika ni kuwa GSM tayari walishamalizana na Coastal Union kilichokuwa kimebaki ni makubaliano na mchezaji ambaye aliomba apewe muda
Mwamnyeto pia anatajwa kuwaniwa na klabu ya Simba