Eymael akerwa na adhabu za kushitukiza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jun 2020
Eymael akerwa na adhabu za kushitukiza

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amekifananisha na hujuma kitendo cha TFF kumfungia nyota wake winga Bernard Morrison muda mchache kabla ya mchezo dhidi ya Namungo Fc

Jana TFF ilitangaza kumfungia Morrison michezo miwili kufuatia tukio alilofanya mwezi Februari na hivyo kukosa mchezo dhidi ya Namungo Fc pia atakosa mchezo dhidi ya Ndanda ambao utapigwa Jumamosi

Eymael ameeleza kushangazwa na adhabu hiyo ambayo uamuzi wake umechukua zaidi ya miezi minne huku pia akibainisha kuwepo kwa matukio mengine ambayo yalifanyika tangu mwezi Januari lakini hakuna hatua zilizochukuliwa

"Jambo hili linasikitisha kwani limekuja wakati tukiwa kambini muda mchache kabla ya mchezo wetu dhidi ya Namungo. Imetushangaza kwa nini maamuzi haya yamechukua muda mrefu, lakini pia yapo makosa yalitokea mwezi Januari kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba lakini hakuna hukumu yoyote," alilalamika Eymael

Aidha adhabu kama hiyo alipewa kiungo wa Simba Jonas Mkude, lakini mchezaji huyo hataathirika nayo kwa kuwa wiki iliyopita klabu yake ilitangaza atakuwa nje kwa wiki mbili kutokana na majeruhi

Mapema leo Kamati ya Nidhamu pia imetangaza kumfungua michezo mitatu beki Lamine Moro

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’