Molinga azikataa 'noti' za mashabiki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jun 2020
Molinga azikataa 'noti' za mashabiki Yanga

Jana Mcongomani David Molinga alikuwa shujaa wa Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc baada ya kufunga mabao mawili muhimu yaliyoinusuru Yanga na kipigo kutoka kwa Namungo Fc

Wakati anaingia kwenye dakika ya 56 kuchukua nafasi ya Mapinduzi Balama, mashabiki wachache walisikika wakimzomea

Hata hivyo mabao yake mawili yaliwapunguzia machungu ambayo wangeyapata kama mchezo ungemalizika kwa kipigo

Sasa baada ya mchezo kumalizika baadhi ya mashabiki walionyesha furaha yao kwa Mcongomani huyo huku wengine wakidirika kumpa pesa ukiwa ni utamaduni wa mashabiki wa Yanga pale mchezaji anapofanya jambo la kuwafurahisha

Hata hivyo Molinga aligoma kupokea fedha hizo lakini pia akigoma kupiga picha na mashabiki wengine waliokuwa wakiomba 'selfie'

Molinga alisikika akilalamika kuwa mashabiki haohao ambao wamekuwa wakimwandama kila siku kuwa hana hadhi ya kucheza Yanga

Wakati anashangilia bao lake la pili alilofunga kwenye dakika ya mwisho kabisa ya mchezo, Molinga alishangilia kwa namna ya kuwafunga midomo wakosoaji wake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’